SMZ MESEMA HAINA NIA YA KUMKOMOA WANANCHI BALI INASIMAMIA NA KULINDA ASILIMALI

serikali  ya mapinduzi ya zanzibar imesema haina nia ya kumkomoa wananchi bali inasimamia na kulinda  rasilimali zilizopo katika kudhibiti uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uchimbaji wa mchanga.

akijibu hoja katika baraza la wawakilishi juu ya bajeti ya  wizara ya kilimo maliasili, mifugo na uvuvi   waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais mh. Aboud Muhammed amesema uamuzi wa kuzuia uchimbaji wa mchanga sio wa wizara ni maamuzi ya serikali katika kuhakikisha maeneo ya ardhi yanatumiwa kwa usalama.

nao baadhi ya mawaziri wamesema kuwa uchimbaji wa mchanga kiholela  umesababisha kukosekana maeneo ya kilimo na mengine hutuwama maji wakitolewa mfano eneo la mwanakwerekwe ambalo limekuwa sikisababisha maafa makubwa hasa katika kipindi cha mvua..

kwa upande wake waziri wa kilimo maliasili, mifugo na uvuvi   mh. Hamad Rashid amesema serikali haijavamia eneo la mtu yeyote ila inatekeleza utaratibu wa matumizi ya ardhi kwa mujibu wa sheria.

aidha ameeleza kuwa kuna baadhi ya wananchi wanatumia hadaa katika biashara ya mchanga kwa kupandisha bei ya juu kuliko iliyotangazwa za serikali

wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepitisha bajeti ya hiyo   ya mwaka wa fedha 2017/2018.