STONE TOWN IMEWAZAWADIYA TUNZO MAALUM WACHEZAJI WAKE

 

Mabingwa  wa ligi kuu ya mpira wa kikapu zanzibar kwa wanaume timu ya stone town  imewazawadiya  tunzo maalum wachezaji wake baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu.

Huo unakuwa ni ubingwa wa 9 katika historia ya timu hiyo kwenye mchezo wa mpira wa kikapu zanzibar tangu kuanzishwa timu hiyo mwaka 1994.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa zawadi hizo katibu wa baraza la michezo zanzibar maalim khamis  ali mzee amesema ni hatua kubwa na ya kipekee iliyofikiwa na timu hiyo katika mafanikio ya mchezo wa kikapu na kuahidi kuwa baraza la michezo litaendelea kushirikiana vyema na vilabu vya michezo kuona maendeleo ya michezo yanakuwa kwa haraka

Naye mwenyekiti wa timu  hiyo  islam ahmed  amesema siri kubwa ya mafanikio ya timu hiyo ni kuendelea kudumisha nidham ya mchezo pindi wakiwa katika ushiriki wa mashindano hayo

Nae fuad rashid ni nahodha wa timu ya stone town sports club na hapa anaelezea furaha ya kuwa mabingwa  wa basketball  zanzibar

Zawadi zilizokabidhiwa kwa wachezaji hao ni ngao maalum pamoja na vyeti kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa kuendeleza historia ya timu yao.