SUALA LA MICHANGO KATIKA SEKTA YA ELIMU LIMETAFSIRIWA VIBAYA

 

Naibu waziri wa elimu mafunzo ya amali mmanga mjengo mjawiri amesema suala la michango katika sekta ya elimu limetafsiriwa  vibaya kinyume  na  kusudio  la  serikali.

Akizungumza katika mkutano wa kuangalia namna ya kuimarisha elimu nchini amesema serikali bado inahitaji ushirikian kuiinua  sekta  ya  elimu  kwa kusaidia baadhi ya huduma za elimu.

Akizungumza  katika   mkutano  huo spika  mstaafu wa  baraza  la  wawakilishi pandu ameir kificho amesema suala la utoro kwa wanafunzi linahitaji juhudi za ziada kukabiliana nalo  kwa kushirikiana na wazazi ili kuweza kubaini mambo mengine zaidi yanayochochea  tatizo hilo kwa wanafunzi.

Washiriki wa mkutano huo wameeleza sababu za  kushuka kwa kiwango cha elimu kuwa  ni pamoja na uhaba wa vifaa, ukosefu wa waalimu kwa fani za sayansi na kuelezea njia za kutatua tatizo hilo