SULTAN ABDULRAHMAN (SULTAN KING) AMEKABIDHI MSAADA KWA WATOTO YATIMA

 

Kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa msanii wa muziki wa kizazi kipya zanzibar, sultan abdulrahman  (sultan king) amekabidhi msaada kwa watoto yatima wanaoishi katika nyumba ya kulelea watoto mazizini.

Msanii huyo akiambatana na  mashabiki wake alitinga ndani ya nyumba hiyo majira ya saa nne za asubuhi, na kukabidhi fedha pamoja na chakula, katuni za maji na juice na vifaa vya kusomea.

Akizungumza na vyombo vya habari, sultan king, amewataka wasanii kujali maisha ya watoto kwa kuwapatia msaada kila inapowezekana kwani ulezi ni wa wote.

Mkuu wa nyumba ya kulelea watoto bi saida ali, amelezea kuridhishwa na uzalendo wa msanii huyo ambao umelenga kuimarisha maisha ya kizazi cha baadae.

Pause msanii sultan king anatarajiwa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa tarehe sita januari.