SUZA TV KUANZISHA VIPINDI VYA MASOMO YA ZIADA KWA MASOMO YA SAYANSI

Chuo kikuu cha taifa zanzibar suza kupitia suza tv itaanzisha vipindi vya masomo ya ziada kwa masomo ya sayansi ili kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya vizuri mitihani ya taifa.
Makamu mkuu wa chuo cha suza prof. Idriss ahmed rai amesema hayo katika mahafali ya nne ya sekondari ya suza
Amesema lengo la suza kuandaa vipindi hivyo ni kuwasaidia wanafunzi na kuwapunguzia wazee gharama ya kuwalipia wanafunzi masomo hayo
Mkuu wa idara ya elimu ya sekondari maalim abdalla ali abeid amesema katika miaka michache ijayo zanzibar itapunguza tatizo la wataalamu kutokana na wanafunzi wa suza kufanya vizuri mitihani ya taifa na kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya zanzibar
Mwanafunzi wa suza sumaiye mohd amesema licha ya kufanya vizuri katika mitihani na kupata nafasi ya 38 kwa tanzaania na nafasi ya pili kwa zanzibar, wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa walimu wa somo la fizikia na vifaa vya maabara.