TAALUMA JUU YA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA RED CROSS KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wamehimizwa kutoa msukumo wa kimaendeleo kwa kuongeza nguvu za ushirikiano na chama cha msalaba mwekundu red cross ili kuimarisha huduma za kijamii nchini.
Katika mkutano wa kutoa taaluma juu ya shughuli zinazofanywa na red cross kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi, rais wa red cross mwadini jecha, amewaeleza wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa wana nafasi kubwa katika kusimamia huduma zonazotolewa na taasisi hiyo ya kimataifa ili ziweze kuwafikia wananchi bila kujali itikadi za kidini na kisiasa.
Amesema kuanzishwa kwa red cross kulikuwa n a nia ya kusaidia kutoa huduma wakati yanapotokea maafa, lakini sasa imejiiimarisha kutoa huduma za kijamii wakati wa amani.
Akitoa mada kuhusu kipaumbele cha mipango mikakati ya red cross katibu mkuu wa taasisi hiyo julius kejo amesema wanapata ushirikiano na mashirika mbalimbali ili kusaidia kufanya shughuli zao kwa haraka na wepesi zaidi.
Nao wajumbe wa baraza la wawakilishi wameiomba tasisi hiyo kujenga mfumo wa kutoa taaluma kwa jamiii juu ya kujikinga na maafa ili yanapotokea yasisiweze kuleta hasara kubwa.
Mkutano huo wa siku moja umefunguliwa na naibu spika wa baraza la wawakilishi mh.mgeni hasssan juma ambae amewataka watendaji wa red cross kuimarisha huduma zao kwa jamiii kila zinapohitajika