TAALUMA JUU YA USAJILI WA NDOA NA TALAKA

 

Wakaazi  wa  shehia  ya   magogoni  wameomba  kupatiwa  taaluma  zaidi  juu  ya  usajili  wa  ndoa   na  talaka  ili  kuwa na mwamko wa kuwasilisha taarifa zao.

Wakitoa  maoni  yao  katika  mkutano wa  wazi   kuhusu  ushiriki  wa  wananchi  katika  kuendesha  serikali  za  shehia   wamesema  itasaidia kutoa  ushirikiano  katika utoaji  wa  vyeti  vya uhakika.

Kwa  upande  wa  shehia  wataweza  kutambua  majukumu yao   na    dosari  zinavyojitokeza  katika  ushirikishwaji  wa  miradi  ya  maendeleo  ndani  ya  shehia.

Kwa  upande  wake  mwanasheria  kutoka  jumuiya  ya  wanasheria  wanawake  zafela zainab  khamis  amesema  inapaswa  wakaazi  wa  kila  shehia  kujisajili  ili kupatikana  taarifa  zinazojitosheleza  kwa  kuiwezesha  serikali  kuu  kupanga  mipango yake.

Mratibu  wa  mradi  huo  nd mbarouk  said  amesema  lengo  ni  kuwawezesha  wananchi  kujua  nafasi  zao katika shehia  ili  kuhakikisha wanashirikishwa  vyema  katika  mipango  ya  miradi  yao.