TAASISI BINAFSI ZINAZOTOA AJIRA ZINASAIDIA KUPUNGUZA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI

 

Waziri wa kazi, uwezeshaji wazee, vijana, wanawake

Na watoto Mhe, Modline Castico amesema taasisi binafsi zinazotoa ajira kwa vijana kunasaidia kupunguza vitendo vya uvunjifu wa amani katika jamii.

Akizindua  mpango wa mafunzo   kazi  katika hotel ya sea  clif iliopo kama waziri huyo kwa amesema idadi ya vijana wasio nakazi inaongezeka kila mwaka huku serikali ikiwa haina  uwezo wa kuwaajiri wote na kwamba kuwepo kwa taasisi kunaipungunzia mzigo serikali.

Amesema serikali ya mapinduzi  zanzibar kwa kushirikiana na wadau mabli mbali likiwemo shirika lakazi duniani  ilo imeweka mikakati  maalum ya kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini kwa kutoa mafuzo  ya kuwajengea uwoze wa kuingia katika soko la ajira vijana.

Mkurugenzi  taasisi ya   utalii wa  chuo kikuu cha  taifa suza   Dr Aleiy  Soud  Nasor     mesema  wanafunzi watakao maliza  katika  chuo  hicho wataweza  kutambulina  na kupata  ajira  kwa uhakika.

Baadhi  ya  wanafunzi  wanaosoma hicho  kupitia   program ya mpango  wamesema  imewasaidi sana  kuondokana na tatizo  la ajira  Zanzibar