TAASISI MBALIMBALI ZIMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KWA HUDUMA ZA KIJAMII NCHINI.

 

 

Mkuu wa wilaya ya mjini bi marina joel tomas amezitaka taasisi mbalimbali nchini kushirikiana na serikali kusaidia kupatikana kwa huduma za kijamii nchini.

Akizungumza wakati akigawa msaada kwa watu walioathirika na mvua za masika uliotolewa na shirika la red cross katika skuli ya msingi sebleni bi marina amesema serikali inaendelea na mradi wa uchimbaji wa mitaro ili kuondosha tatizo la kujaa maji kwa baadhi ya maeneo  katika mkoa wa mjini magharibi.

Naye mratibu wa shirika la red cross nd. Ubwa suleiman amewataka wananchi kuwa na tahadhari wakati wa mvua zinapoanza kunyesha ili kuepukana na matatizo.

Misaada hiyo imekabidhiwa kwa shehia ya sebleni kwa wazee, sogea, saateni, kilimahewa na amani.