TAASISI YA JAMIIYATUL ISLAAM YA ZANZIBAR INATARAJIA KUWEKA KAMBI

 

 

Taasisi ya Jamiiyatul Islaam ya Zanzibar  inatarajia kuweka kambi ya kuchunguza maradhi mbali mbali kwa wananchi wa Zanzibar i inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa taasisi hiyo mmanga nassor amesema lengo la kuweka  kambi hiyo    kuwasaidia wananchi ambao  hawawezi kumudu gharama za matibabu

Amesema huduma za uchunguzi zitakuwa bila ya malipo  kwa wananchi wote wa zanzibar ambapo watapata fursa ya kuchunguzwa maradhi saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti , shindikizo la damu pamoja na uchuguzwa wa ma tibabu ya meno .

Nae Daktari naeshughulikia taasisi hiyo Soudi Mgaya amesema katika uchunguzi kutakuwepo na madaktari bingwa kutoka Tanzania Bar na  Zanzibar ambao watachunguza afya za wananchi na kupatiwa matibabu kwa wale watakao baini ka maradhi.

Waziri wa afya Mhe Hamadi Rashid Mohamed ameitaka taasisi hiyo kuzingatia utoaji wa matibabu kwa wale wagonjwa watakao bainika kugundulika na maradhi sambamba na kuwapata dawa za matibabu.

Aidha ameishukutu tasisi hiyo kwa kuweza kujitolea kwa kutoa huduma za uchunguzi  maradhi kwa wananchi wa Zanzibar kwani kufanya hivyo kutaweza kuisaidia serikali katika utoji wa huduma za afya kwa wananchi wake.