TAASISI YA MANISPAA IPO TAYARI KUFANYIA MATENGENEZO MAJENGO YA SKULI YA CHUKWANI NA KISAUNI

 

 

Mkurungenzi wa manispaa ya magharibi’b’  nd. Amour ali mussa, amesema  taasisi yake iko tayari  kufanyia matengenezo majengo  ya skuli ya chukwani na kisauni  ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.Akitembelea katika skuli ya kisauni na chukwani  amesema   atahakisha mabanda ya kusomea wana funzi yanamalizika kwa wakati ili wanafunzi wasome kwa  uzuri na wafaulu  vizuri.

Mwakilshi wa jimbo la chukwani mh  mwanasha  khamis amesema    madarasa  ya chukwani yamekuwa yakivuja  ambapo wanafunzi wanapata tabu hivyo kupitia  mashirikiano na halmashauri watajitahidi  kuyatengeneza upya  madarasakwa upande wa  madiwani  na naibu sheha wameelezea   jinsi wanafunzi wanavyopata tabu hasa kipindi hiki cha mvu kwa kurudikana darasamoja na kuiomba  kuharakishwa ili wanafunzi  wasome kwa wakati.