TAASISI YA NYARAKA KUJENGEWA JENGO LA KISASA

 

Taasisi ya nyaraka na kumbu kumbu zanzibar inakusudia kupeleka maombi serikalini, kutaka kujengewa jengo la kisasa litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi nyaraka katika hali ya usalama zaidi.

Jengo hilo lenye umuhimu mkubwa kwa taifa kwa liliopo kilimani mjini unguja kwa sasa limezungukwa na makaazi ya watu hali ambayo imemlazimu mkurugenzi wa taasisi hiyo nd. Salum suleiman salum, wakati wa ziara ya ujumbe kutoka nchini oman, kuelezea dhamira hiyo ya kutaka jengo jipya kwa lengo la kuimarisha usalama  kumbu kumbu za taifa.

Amesema mbali na makaazi ya watu pia kuna madhara ambayo yanaweza kusababishwa na baadhi ya wanyama waharibifu hasa kutokana na mazingira ya eneo hilo lilivyo.

Kuhusiana ziara hiyo ya ujumbe wa oman katika taasisi hiyo itasaidia kubadilishana uzoefu wa kiutendaji na kuangalia uwezekano wa kuwaongezea taaluma ya kiutendaji wafanyakazi wake.

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na waziri wa habari, utalii na mambo ya kale mh. Mahmoud thabit kombo, pamoja na mengine ujumbe huo wa oman ukiongozwa na katibu mkuu wizara ya urithi na utamaduni  nchini oman bw salu mohamed  almahrouk, ulipata maelezo kuhusiana na utunzaji wa nyaraka na kumbu kumbu za serikali.