TAASISI YA ZANZIBAR MILELE FOUNDATION KUENDELEA KUWA NA UMOJA NA USHIRIKIANO

 

Mkuu  wa mkoa wa mjini magharib mh ayoub mohamed mohamoud  ameitaka  taasisi ya zanzibar  milele foundation kuendelea kuwa na umoja na kushirikiana katika kuleta maendeleo nchini.Akizungumza katika ukumbi wa grand palece  amesema njia nzuri ya ushirikiano ni umoja na upendo miongoni mwetu ndio lengo linaweza kufikia.Mh ayoub jamii ya zanzibar ina umoja wa kufutari kwa pamoja ndio ngao ya kujenga udugu na kuendeleza utamaduni  mila na silka  za wa wazee  walioziwacha hivyo hakuna budi kufuatwa utamaduni huo.Hata hivyo mh ayoub  amewataka wananchi  kuendeleza  amani na utulivu kwani  ndio msingi wa  maendeleo.Mkuu wa utawala wa zanzibar milele   foundation  kassim mbarouk  amesema milele imejipanga  kuweka mpango mkakati   ambao  utaimarisha ustawi  wa  jamii  na  kuendelea kuleta maendeleo  katka  njanja  bali mbali  nchini.