TAASISI ZA KIRAIA ZINAZOTOA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA KUWA MAKINI

 

Akifungua mafunzo ya kuimarisha mabaraza ya vijana kupitia sera za kitaifa mkoa kaskazini unguja, katibu tawala wilaya kaskazini ‘b’ juma abdallah hamad, amesema ufuatiliaji utawezesha  kuwazindua vijana hao kuwa makini na kuifikisha kwa wengine taaluma waliyopatiwa.

Mratibu wa mradi huo khamis hassan kheir, pamoja na viongozi wa mabaraza ya vijana wamesema wamejipanga kuona wanayafanyia kazi kwa vitendo mafunzo wanayopatiwa, kwani yamelenga kuwajengea mazingira ya kuwa viongozi bora.

Mafunzo hayo yameandaliwa mtandao wa asasi za kiraia mkoa kaskazini unguja kwa ufadhili wa the foundation for civil society ya dar es salaam.