TAASISI ZA SERIKALI IMEOMBWA KUELEKEZA NGUVU ZAO KATIKA JUMUIYA ZINAZOSAIDIA YATIMA

 

Taasisi za serikali na mashirika binafsi zimeombwa kuelekeza nguvu zao katika jumuiya zinazosaidia yatima ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.Akizungumza katika utoaji wa sadaka kwa watoto yatima huko msikiti mushawal mwembeshauri , mwenyekiti wa jumuiya ya kusaidia wagonjwa na ustawi wa jamii zanzibar sheikh abuubakar haji rubeiya amesema iwapo taasisi hizo zitasaidia jumuiya hizo zitaweza kutoa misaada mbalimbali kwa yatima na wagonjwa.

Amesema bado kuna baadhi ya taasisi hazijahamasika kutoa michango yao itakayowawezesha yatima na wagonjwa kuona nao wanathaminiwa katika jamii. Nao viongozi wa jumuiya hiyo wamefahamisha kuwa ni vyema kwa jamii kutekeleza wajibu wa kuwatunza na kuwaenzi yatima ili waweze kuishi kwa amani bila ya kunyanyasika.