TAASISI ZA SERIKALI KUCHAPISHA MACHAPISHO YAO KATIKA SHIRIKA LA WAKALA WA UPIGAJI CHAPA
Taasisi za serikali zimetakiwa kuitikia wito wa serikali kwa kuweza kuchapisha machapisho yao katika shirika la wakala wa upigaji chapa ili kuweza kuingizia serikali mapato.Mkurugenzi mkuu wakala wa upigaji chapa mohamed suleiman, amesema hayo katika ziara za viongozi walio chini ya wizara ya habari, utalii na mambo ya kale, walipotembelea katika taasisi hiyo na kujionea hali halisi ya utendaji kazi katika shirika hilo .
Amesema shirika lake limeweza kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zake kwa kuweza kuzalisha bidhaa mbali mbali kwa lengo kuongeza soko la nje na ndani nchinNae meneja uendeshaji wa kiwanda hicho isaac muturi, amesema kiwanda hicho kinauwezo wa kuchapisha machapisho mbali mbali yakiwemo ya serikali na watu binafsi ambapo kwa siku wana uwezo wa kuchapisha zaidi ya vitabu elfu tano.Meneja masoko katika shirika la wakala wa uchapaji khanat mohamed aboud, amesema soko la uuzaji wa bidhaa linazidi kukua kutokana na kujitangaza katika maonesho mbali mbali ya kibishara.Naibu katibu wa wizara ya habari anaeshughulikia utalii na mambo ya kale, dk amina ameir, ameupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kufanya kazi zao vizuri na kuweza kujitangaza kibishara ndani na nje ya nchi.