TAASISI ZA VIWANGO ZANZIBAR KUZINGATIA UMUHIMU WA VIWANGO

 

Naibu katibu mkuu wizara ya biashara viwanda na masoko Ali Khamis Juma  amewataka wanakamati wa taasisi za viwango Zanzibar kuzingatia umuhimu wa viwango kwani mahitaji yake ni makubwa Zanzibar.

Akifungua mafunzo maalum kwa wanakamati wa viwango Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi naibu katibu mkuu huyo amewataka wanakamati hao kusimamia viwango kwa uzoefu walionao ili visaidie kumlinda mtumiaji.

Katibu mkuu wa shirika la viwango afrika Hermogene Nsengimana akiwasilisha mada katika mafunzo hayo ya wajibu wa kitaalamu wa kamati za viwango amesema mafunzo hayo yatawasaidia wanaosimamia ubora wa bidhaa kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya viwango zanzibar khatibu mwalim ameelezea lengo la mafunzo hayo ni kupeana maelekezo yatakayosaidia katika kazi za uaandaaji wa viwango na kuwaongezea taaluma wanakamati.

Mafunzo hayo yamewashirika wanakamati wa viwango zikiwemo kamati ya viwango vya kemikali na bidhaa za kemikali, kamati ya kitaalamu ya viwango vya mazingira na kamati ya kitaalamu ya viwango vya chakula na bidhaa za chakula