TAASISI ZENYE UWEZO ZIMETAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI WASIO JIWEZA

Taasisi zenye uwezo zimetakiwa kujitokeza kuwasaidia wananchi wasio jiweza na wale walipatwa na maafa ya mvua hasa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Ushauri huo umetolewa na wakazi wa kijiji cha chokocho ngezi na kisiwa paza baada ya kupatiwa misaada kutoka taasisi ya all ikhlas charita bul group inayoongozwa na mfanya biashara said nasir bopar
Wakaazi hao wamesema misaada hiyo itawasaidia kujikimu kimaisha kutokana na wengi wao mazoo yao kuathirika na mvua.
Wawakilishi kutoka taasisi hiyo wamesema wataendelea kutoa misaada zaidi ili kusaidia jamii iliyopatwa na maafa