TAASISI ZIMETAKIWA KUYATAFUTIA HATI MILIKI MAENEO YA MISITU

 

Katika kuhifadhi maeneo ya misitu yasivamiwe kwa shughuli mbali mbali za kibinadamu, taasisi zinazohusika zimetakiwa kuyatafutia hati miliki maeneo hayo ili kuifanya zanzibar kuendelea kuwa yenye haiba ya kijani.Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo, maliasili mifugo na uvuvi nd. Ahmad kassim amesema wizara imekuwa na mkakati wa kuendelezwa misitu kwa kupanda miche mingi zaidi hivyo ni jukumu la kuhakikisha maeneo hayo hayavamiwi ili kuongeza uzalishaji.

Katibu mkuu huyo alikuwa akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha utafiti na mafunzo mwanyanya pamoja na kuwaaga wafanyakazi waliostafu kutoka idara ya misitu ambapo amesema jamii iendelee kuhamasishwa kupanda miti kwa hiyari kutokana na umuhimu wake kwa mahitaji ya mwanadamu.Mkurugenzi idara ya misitu na rasilimali zisizorejesheka nd. Soud soud mohamed juma ameiomba wizara ya kilimo kuiongezea nguvu ya kisheria idara hiyo katika kusimamia usalama wa misitu isiharibiwe kwa makusudi.Wafanyakazi waliostaafu wamesema ujuzi walionao katika kuotesha na kusimamia vitalu vya miti mbalimbali wataumia kuhasisha jamii kupanda miti katika maeneo yao.