TAHADHARI IMETOLEWA KUDHIBITI JENGO KONGWE LILIOPO LA FORODHANI KUHAKIKISHA USALAMA

Wakati   ujenzi wa   ukuta    pembezoni   mwa   ufukwe   wa   forodhani   ukiendelea   tahadhari  imetolewa   ya  kuchukuliwa hatua za haraka  kudhibiti jengo kongwe  liliopo   eneo   hilo  ili  kuhakikisha    usalama

Wa  vyombo  vya   usafiri   na    wapita   njia.

Jengo hilo la  miaka  mingi  linaloonekana kuwa  katika  hali  mbaya  ya    uchakavu   mbali   na  kuondosha   haiba   ya  eneo   hilo  pindi   ukuta   wa   bahari   na  barabra  utakapokamilika.

Makamo   mwenyekiti   wa bodi  ya  mamlaka   ya   mji  mkongwe   Saleh   Sadiq   akiambatana   na   wajumbe   wa  bodi   hiyo   ameshauri  kuchukuliwa    hatua  z a  ufumbuzi   ikwemo   kufanyiwa  ukarabati  pamoja  na   kuezekwa   kwa   lengo  la    kuwa   na    usalama.

Mmiliki  wa   jengo   hilo  hamid    abdulhamid  amesema    hana  pingamizi    lolote   na   yuko    tayari   kuona    jengo    hilo   linafanyiwa   matengenezo  kwa   kuwa    linahitaji   gharama   kubwa

Mkurugenzi  wa   mamlaka   ya  mji mkongwe   issa makarani  sariboko  amesema   tayari   mamlaka imewasilisha    gharama   za   uezekaji  wa   serikalini zinazofikia  takriban   shillingi    milioni   65 .