TAIFA LINATEGEMEA WATAALAMU ILI WAWEZE KUSAIDIA KUHARAKISHA MAENDELEO YA NCHI.

 

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekti wa Baraza la Mapinduzi dk. Ali Mohd Shein amesema  pamoja na  kuwepo  wasomi wengi kutokana na   kuongezeka kwa vyuo vikuu nchini  bado taifa  linategemea   wataalamu  kwa  michango yao ili waweze kusaidia kuharakisha  maendeleo ya nchi.

Amesema  kutokana na mafanikio hayo    serikali imekuwa ikiunga mkono  shirika la kiislamu linalotoa misaada afrika kwa kuelekeza misadaa yake katika maendeleo ya elimu

Dk. Shein ameeleza   hayo  kupitia  hotuba yake iliyosomwa na naibu waziri wa elimu na mafunzo ya amali  mh mmanga mjengo mjawiri  katika mahafali ya 17 ya chuo kikuu cha sumeit yaliyofanyika chukwani.

Amesema  kutokana  na  chuo kikuu cha sumeit  kushika  nafasi ya 31 kwa tanzania huku  kwa afrika kikishika nafasi ya 200 kwa ubora  hivyo   kinahitaji kufanya  juhudi za ziada  katika kuhakikisha  kinajijengea nafasi nzuri zaidi ya ubora wa kutoa elimu kwa kufundisha.

Hata hivyo dk. Shein amevikumbusha   vyuo vikuu hapa zanzibar kwa kusema  kuwa  vina umuhimu mkubwa wa kuikuza  lugha ya kiswahili  ili kusaidia  malengo ya kamisheni ya kiswahili ya afrika mashariki  ambapo zanzibar imechaguliwa kuwa makao makuu ya lugha hiyo.

Akizungumza  kwa niaba ya rais mh  mjawiri amesema   hotuba hiyo pia imezingatia  umuhimu  na  ubora  wa elimu na viwango ili wahitimu waweze kuingia katika ushindani wa soko la ajira hapa nchini.

Makamo mkuu wa chuo  kikuu  sumeit dk. Hemed rashid hikman  amesema mwaka huu wamejiwekea mikakati    kwa   kuanzisha kampas nyengine  za masomo mbali mbali   ikiwemo masomo ya sayansi.

Amewataka  wahitimu hao  kujijengea mazingira mapya  ya kubadilika katika   utumishi wao pale watakaporejea makazini mwao.

Awali balozi mdogo  nchini  kuweiti  tanzania  dk. Muhammad rashid alamir ameishukuru serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa  jitihada inazochukuwa katika kuungamkono  jitihada za elimu   na kusema  kwamba zinaimarisha ushirikiano na urafiki.

Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa vyeti ni pamoja na ngazi ya  shahada,cheti , diploma, digeree