TAKRIBAN TANI 1.6 ZA BIDHAA MBALI MBALI ZA VYAKULA ZIMETEKETEZWA

Takriban tani 1.6 za bidhaa mbali mbali za vyakula ambazo hazifai kwa matumizi ya wanaadamu zimeteketezwa na bodi ya chakula na dawa zanzibar

akitoa ufafanuzi wa zoezi hilo kaimu mkurugenzi mtendaji wakala wa chakula na dawa Zanzibar Dr Khamis Ali Omar amesema bidhaa zote hizo zilizoteketezwa zimetoka katika makampuni mbali mbali nchini baada ya wamiliki wa kampuni hizo kuona bidhaa zao hazifai kwa matumizi ya binaadamu kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuishiwa na muda wa matumizi.

amesema bodi ya chakula na dawa inawataka wafanya biashara wanapoona bidhaa zao hazifai ni vyema wakatoa taarifa ili kuweza kufanyika taratibu za kuziteketeza bidhaa hizo kabla ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.

aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wafanya biashara wasio waaminifu katika uingizaji na uuzaji wa bidhaa zisizokubalika ili ziweze kuchukuliwa hatua za haraka kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa zenye usalama.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App