TANI 200 ZA MCHANGA UNAOSADIKIWA KUCHIMBWA BILA YA KIBALI ZIMEKAMATWA

 

Zaidi   ya  tani 200  za  mchanga  unaosadikiwa  kuchimbwa  bila  ya kibali  katika  maeneo  yasiyo  rasmini  zimekamatwa  na  uongozi  wa wilaya  kaskazini  ‘a’  katika  viwanda  vya matofali  maeneo  tofauti.

Wakiwa katika  ziara  ya  kawaida  ya  kukagua  maeneo  yanayo chimbwa  mchanga  bila ya ruhusa  ya  serekali  ya  wilaya na uongozi  wa halmashauri,  katibu  tawala  ya wilaya  ya kaskazini ‘ a’  mohamed  omar  na afisa  misitu  na  rasilimali  zisizorejesheka  mgwali  makame,  wamesema uongozi  wa  wilaya  umechukua  hatua  ya kuvifungia  viwanda hivyo  kutofanya  kazi  ili  kuruhusu  uchungizi  wa tukio hilo.

Wamiliki  wa  viwanda  hivyo  wamekiri  kuletewa  mchanga  huo  wakati  usiku  ila   hawana  taarifa  yoyote  ya  kuibiwa  kwa  mganga huo   kwani  wameununua   kwa  bei  ya kawaida.

Mchanga  huo  unaosadikiwa  kuchimbwa  usiku  wa  kumkia  jana  umegundulikana  kutokana  na  kulinganisha  na  mchanga  unao chimbwa  katika  shimo  la  serekali  na  shimo  linalodaiwa  kuchimbwa  mchanga  huo  kuwa  ni  tafauti.

Hata hivyo  wameiomba serekali  kutowachukulia  hatua kubwa   za kisheria kwani  wana familia  na kujiajiri  wenyewe  bila ya kutegemea ajija serekalini.