TANI NANE ZA SAMAKI ZIMESHUSHWA BANDARINI KWA AJILI YA UNUNUZI KWA WAFANYABIASHARA

Tani nane za samaki zimeshushwa bandarini zanzibar kwa ajili ya ununuzi kwa wafanyabiashara na matumizi ya kawaida.
Kushushwa kwa samaki hao hiyo inatokana na ushirikiano baina ya mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu campuni za uvuvi zilizo pewa kibali hivi karibuni.
Lengo ni kupunguza bei ya samaki kwa watumiaji pamoja na kufaidika na rasilimani zitokanazo na uvuvi wa bahari kuu.
Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa rasilimali kutoka mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu nd christian nzowa amesema ushushwaji na uzwaji wa samaki utapunguza gharama za ununuzi wa samaki nchini.
Mfanya biashara kutoka kampuni ya zanchick ambae amenunua tani sita za samaki hao nd issa kassim issa amesema hatua hiyo itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa samaki nchini na kuimarisha hali ya samaki.