TANZANIA INATHAMINI UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA, KISIASA, KIUCHUMI WA CUBA

Waziri mkuu kassim majaliwa amefanya mazungumzo na makamu wa rais wa cuba, bi. Gladys bejarano na kumuhakikishia kuwa watafungua ofisi za ubalozi wa tanzania nchini humo ili kurahisisha utendaji wa kazi za kibalozi.
Amesema tanzania inathamini uhusiano wa kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiafya na kiutamaduni na nchi hiyo yaliyokuwepo kuanzia serikali ya awamu ya kwanza.
Pia waziri mkuu ameishukuru serikali ya cuba kwa ujenzi wa kiwanda cha dawa za kuulia wadudu wa maralia pamoja na ufadhili wa masomo ya udaktari kwa wanafunzi wa kitanzania wanasoma nchini humo na kuimba kuendelea kuwafadhili kwa masomo ya ngazi ya shahada ya uzamili.
Kwa upande wake, bi. Gladys amesema serikali ya cuba itaendelea kushirikiana na tanzania katika kuimarisha sekta za afya, utamaduni, kilimo, uchumi na elimu.
Balozi wa tanzania nchini canada anasimamia na nchi ya cuba, balozi jack zoka amesema serikali ya cuba ni miongoni mwa nchi zinazoshirikiana na tanzania katika kuimarisha shughuli za maedndeleo, hivyo uwepo wa ofisi za ubalozi nchini humo utazidi kuimarisha mahusiano.