TANZANIA INAUNGANA NA MATAIFA MENGINE KUADHIMISHA SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya mabaharia duniani ili kuonesha mchango wa watu hao katika kukuza maisha ya wananchi na uchumi wa tanzania.
Maadhimisho hayo ya siku mbili kutafanyika maonesho ya taasisi mbali mbali za ubaharia tanzania yatafunguliwa makamo wa pili wa rais balozi seif ali iddi nakufungwa na makamo wa rais wa tanzania mhe samia suluhu hassan
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri baharini zanzibar abdullah hussein kombo amesema ujumbe wa mwaka huu ni mtunze baharia kwa kukuza uchumi na maisha ya tanzania kutokana na umuhimu wake katika sekta ya biashara.
akizungumzia maendeleo ya sekta hiyo amesema ingawa tanzania ina nafasi nzuri bado mabaharia wanaojihusisha nayo hawapendi kujiendeleza kielimu na sasa wanaendelea wakiamini kuwa ni kazi isiyohitaji elimu.