TANZANIA NA UGANDA KUZINDUA MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

Rais wa Tanzania dkt. John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda wamezindua mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini uganda hadi bandari ya tanga mkoani tanga.
Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa kilometa elfu moja mia nne 43 utagharimu dola za marekani bilioni 3 nukta 55, na unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya zaidi ya elfu kumi hadi kukamilika kwake.
Rais wa tanzania dkt. John magufuli akizungumza katika uzinduzi huo amesema mradi huo uliofanyika eneo la chongoleani jijini tanga utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi hizo mbili na za afrika mashariki.
Aidha amesema wanaendelea na utafiti wa utafutaji wa mafuta katika ziwa tanganyika na iwapo yakipatikana bomba la kusafirishia litaunganishwa na hilo la uganda.
Kwa upande wake rais yoweri museveni wa uganda amesema mradi huo ni hatau nzuri ya kukukuwa uchumi imarisha uchumi wa nchi hizo mbili ikiwemo kuweza uchakataji wa mafuta ghafi, kuzalisha mbolea, saruji, lami na bidhaa nyingine hatua na kufikisha kasi ya ukuaji wa viwanda.
.