TATIZO LA KUINGIA MAJI KATIKA NYUMBA LINALOTOKANA NA KUJIFUKIA KWA MTARO

 

Wakaazi wa maeneo ya chumbuni  wamelalamikia tatizo la kuingia maji katika nyumba zao linalotokana na kujifukia kwa mtaro uliokua ukipitisha maji hapo awali  kulikosababishwa na mtaro uliochimbwa katika eneo linalotuama maji katika bwawa la maeneo hayo maarufu kwa mzushi.

Wakitoa malalamiko  yao  wakaaazi   hao  wamesema mtaro huo ungejengwa katika njia hiyo iliyokuwa ikipitisha maji hapo zamani ungesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la kuingia maji katika nyumba zao kuliko kuyajengea bondeni na kusubiri maji yafikie huko jambo ambalo yanapita kinyume na matarajio hayo na kuishia katika nyumba zao.

Akisisitiza kuhusu suala hilo sheha wa shehia ya chumbuni nd.hassan juma ameiomba idara inayohusika kutafuta mbinu za kuunganisha mtaro huo uliochimbwa katika eneo la bwawa pamoja na huo uliokuwepo awali ili uweze kutatua matatizo yanayo wakabili wakaazi wa eneo hilo.

Kwa upnde wa uongozi  unaoshughulikia masuala ya ujenzi wa mitaro hiyo wamesema ujenzi usiofuata tararatibu za mipango miji unachangia kwa kiasi kikubwa maji kutofuata njia zake za kawaida.