TATIZO LA MAJI NA WADUDU LAWAKWAMISHA WAJASIRIAMALI

Wajasili ya mali wa vikukndi vya mboga mboga jimbo la kijini wamesema uhaba wa maji na wadudu waharibifu ndio matatizo makubwa yanayo wakabili katika kilimo cha mbogamboga.
Wakizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mitaji kutoka kwa mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo wajasiliamali hao wamesema ingawa wanafanya juhudi ya kujikwamua kimaendeleo lakini bado changamoto hizo zikikwamisha juhudi zao hivyo wamewaomba mbunge na mwakilishi kuwasaidia katika kutatua changamoto hizo
Mbunge wa jimbo hilo mh: makame mashaka fumu amesema serikali zote mbili zinachukuwa juhudi za kuwaletea wananchi wake huduma za kimaendeleo na wataendelea kuboresha huduma kwa jamii hivyo amewataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo ili wajikwamue kimaisha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya kaskazini “a”ali makame khamisi amewataka wanavikundi hivyo kuitumia misada hiyo kwa lengo lililokusudiwa ili kuunga mkono juhudi za serikali.