TATIZO LA MUDA MREFU LA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA SKULI YA FUONI

 

Skuli ya msingi fuoni a  inatarajia kuondokana na tatizo la muda mrefu la upatikanaji wa maji katika skuli hiyo hali iliyokuwa ikiwalazimu wanafunzi kutembea masafa marefu kufuata huduma hiyo.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa huduma hiyo imekosekana, kwa ajili ya matumizi ya huduma za skuli lakini faraja waliyonayo sasa ni baada ya kujitokeza mfadhili kuwajengea kisima katika eneo la skuli.

Viongozi na wadau mbali mbali wa elimu wameelezea faraja yao kwani hata wao walikuwa na wakati mgumu wa kufuatilia ufumbuzi wa tatizo hilo kwani baadhi ya wakati lilikuwa linaathiri masomo kwa wanafunzi kutokana na kulazimika kutafuta maji nje ya eneo la skuli.

Licha ya ufadhili wa kisima hicho, juhudi hizo zimeungwa mkono na viongozi wa jimbo la dimani kwa kutoa fedha za kuweka miundo mbinu ya kufikisha huduma hiyo katika maeneo mbali mbali ya skuli.