TILLERSON ANAKABILIWA NA MAZUNGUMZO MAGUMU URUSI

 

 

Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa marekani rex tillerson mjini moscow itakuwa mtihani wa mwanzo iwapo utawala wa rais donald trump unaweza kutumia msukumo wa aina yoyote unaotokana na shambulio la makombora dhidi ya kituo cha jeshi la anga la syria kuimarisha na kutekeleza mkakati wake wa kumaliza vita vya syria.

Ziara ya tillerson imetarajiwa kuangalia zaidi kuingilia kwa urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016 wa marekani, ikiwa ni ukiukaji dhahiri wa mkataba muhimu wa udhibiti wa silaha, na kuona iwapo ushirikiano unawezekana katika mapambano dhidi ya kundi la dola la kiislamu.

Serikali ya urusi imesema tillerson hajapangiwa kukutana na rais wa urusi vladimir putin katika ziara yake hiyo na badala yake atakutana na waziri mwenzake wa mambo ya kigeni sergei lavrov.