TILLERSON YUKO KUWAIT KUUTATUA MZOZO WA GHUBA YA KIARABU

Waziri wa mambo ya kigeni wa marekani rex tillerson yuko nchini kuwait, ambayo ni mpatanishi mkuu kati ya qatar na jirani zake wa kiarabu kwa ajili ya mazungumzo yenye lengo la kutatua mzozo huo ambao ni mbaya kuwahi kushuhudiwa katika eneo la ghuba.
Tillerson atafanya mikutano nchini kuwait, qatar na saudi arabia hadi alhamis katika kile kinachoonekana kuwa ni hatua ya kwanza muhimu ya marekani katika utatuzi wa mgogoro huo.
Amefanya mazungumzo na mfalme wa kuwait sheikh sabah al-ahmad al-sabah ambaye anaongoza juhudi za upatanishi kati ya mataifa ya ghuba.
marekani na uingereza zilitoa taarifa ya pamoja baada ya mazungumzo ya jana ikiziomba nchi za ghuba kuudhibiti haraka mzozo wa sasa na kuutatua kupitia mazungumzo.