TIMU YA CHEJIO KAZI YA MAKUNDUCHI IMEFANIKIWA KUTWAA UBINGWA

 

 

Timu  ya chejio kazi  ya makunduchi  imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya tam cup 2017 baada ya kuilaza  timu ya  m 23  kwa matuta

Mchezo  huo wa fainali uliokuwa mkali na kusisimuwa   mashabiki waliojitokeza kushuhudia mtanange huo katika kiwanja cha kitenge mzuri makunduchi.

Timu ya chejio kazi iliyovalia jezi rangi bluu  imejinyakulia  ushindi huo baada ya kuwalaza kakazao wa timu ya m 23 kwa matuta 4- 5  kufuatia dakika tisini  za mchezo huo  kushindwa kufungana na kuibua nderemo na kwa mashabiki wao.

Akikabidhi zawadi kwa mabingwa hao mwakilishi wa jimbo la makunduchi  maalim harun ali suleiman amesema viongozi wa jimbo wataendelea kuunga mkono michezo  na kuzipongeza timu zote shiriki za mashindano hayo

Nao wachezaji wa timu hizo wameelezea hali ya mchezo huo  ulivyokuwa

Timu ya chejio kazi  imekabidhiwa kitita cha fedha taslim shilingi laki saba na kombe huku mshindi wa pili timu ya m 23 ikijinyakulia shilingi laki tano