TIMU YA JKU IMEIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 ZIDI YA TAIFA YA JANG’OMBE

Timu ya JKU imeibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri zidi ya taifa ya Jang’ombe katika mechi ya ligi kuu hatua ya nane bora ndani ya dimba la aman.
Bao la jku waliovalia jezi rangi nyekundu limetiwa wavuni na mchezaji m’barouk chande dakika ya 81 baada goli kipa wa taifa ya jang’mbe ahmed ali kushindwa kuuzuia mpira huo na kupelekea kuingia kimiani.
Kutokana na matokeo hayo jku sasa wana shika nafasi ya sita wakati taifa ya jang’ombe wanashika mkia.
Mchezo huo ulikuwa wa kusisimua ambao umeibua hisia za mashabiki wa mpira wa miguu kisiwani hapa.
Makocha wa timu zote mbili waliezea juu ya ugumu mechi hiyo na jinsi matokeo yalivyo kuwa.
Na kwaupande wa pemba uwanja wa gombani jamhuri imetoka kidedea kwa ushindi wa mabao 3 -0 dhidi ya okap.
Ligi hiyo itaendelea tena kwa mzunguko wa tatu,siku ya jumapili jamhuri itapambana na kizimbani saa 10 jioni uwanja wa gombani pemba huku taifa ya jang’obe itakipiga na zimamoto saa 10 jioni kiwanja cha amani.