TIMU YA MASHEHA WA WILAYA YA MAGHARIBI A IMEENDELEZA WIMBI LAKE LA KUCHEZA MICHEZO YA KIRAFIKI

 

 

 

Timu ya masheha wa wilaya ya magharibi a imeendeleza wimbi lake la kucheza michezo ya kirafiki baada ya kucheza na timu ya Viterani wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwajuni timu ya Masheha wa Wilaya ya Magharibi A waliovalia jezi rangi ya kijani walitawala mchezo huo lakini safu yake ya ushambuliaji iliyokuwa butu imejikuta ikipoteza nafasi nyingi za wazi na kulazimika mchezo huo kuishia kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Akizungumza lengo la kuanzisha timu hiyo ya Masheha mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Captain Khatib Khamis amesema lengo la kuazisha timu hiyo ni kudumisha Amani huku akisisitiza timu hiyo itakuwa endelevu.Nae Mselem Haji Mselem ambae ni katibu wa ZFA Wilaya ya Kaskazini A amesema mchezo huo ulikuwa mgumu sana kutokana na kujikumbushia enzi zao huku akimpa tano muamuzi wa mchezo huo.

Nae Issa Ahmada Hijaa Jogoo ambae ni Kocha mkuu wa timu ya masheha wa Wilaya ya Magharibi A amesema timu yake imeonyesha kiwango cha hali ya juu licha ya kuonekana kuwa wazee.Huo ni mchezo wa pili tangu kuanzishwa kwa timu hiyo ya Masheha wa Wilaya ya Magharibi A ambapo mechi yao ya awali walitoka sare ya 3-3 na timu ya Viterani wa Jambiani huku wakitarajia kucheza michezo mengine ya kirafiki mara kwa mara.