TIMU YA SHELA KUTOKEA FUMBA WAMEFANIKIWA KUTWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA HASSAN GHARIBU CUP

 

Timu ya shela kutokea fumba wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya hassan gharibu cup baada ya kuifunga timu ya njugu mawe ya bweleo bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa bweleo.

Ulikuwa mchezo wa fainali ya aina yake ambapo timu ya njugu mawe kutoka  bweleo waliovalia jezi rangi ya bluu walimili mchezo huo lakini bahati haikuwa yao na kupelekea hadi dakika 90 zinamalizika vijana kutoka fumba timu ya shela kutwaa ubingwa huo.

Mara baada ya kumalizika mchezo huo tukafanikiwa kuzungumza na manahodha pamoja na viongozi mbali mbali waliofika kiwanjani hapo wakielezea mchezo huo.