TIMU YA STONE TOWN KUWEZA KUTWAA UBINGWA OPEN CUP LIGI YA MPIRA WA KIKAPU

 

Open cup  ligi ya mpira wa kikapu  wilaya  ya  mjini imeendalee  katika  kiwanja  cha  maisara.

Kwa  kulipngwa mchezo  kati ya ston town   walio valia jezi nyeusi  imefanikiwa kuibuka  na ushindi baada ya kuwafunga  rangers    kwa vikapu 76 dhidi ya 54.

Mchezo huo wa kuvutia pande zote mbili zilijitahidi kuhakikisha wanatoka na ushindi kwa kucheza mchezo nzuri uliowavutia mashabiki wa pira huo.

Stone  ilipania  kuibuka  kidedea  katika  mchezo baada ya  kuwashusha  dimba  nyota  wao  wote  waliotamba  katika  ligi  kuu  ya  zanzibar  msimu uliopita.

Kwa  matokeo  hayo  inaiweka  pazuri  timu  ya  stone town  kuweza  kutwaa  ubingwa  huo  ulioandaliwa na chama cha mpira wa kikapu wilaya ya mjini.