TIMU ZA JKU NA ZIMAMOTO ZIMEKAMILISHA MAANDALIZI YA MICHEZO YAO

 

Wawakilishi wa zanzibar  katika michuano ya vilabu barani afrika  timu za jku na zimamoto zimekamilisha maandalizi ya michezo yao ya kiamataifa itakayofanyika wikiendi hii katika uwanja wa amani.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha matayarisho ya michezo yao ya kimataifa dhidi ya timu watakazo  chuana nazo katika mashindano hayo  katibu mkuu wa timu ya jku saad ujudi  amesema kikosi chao kipo tayari kwa mpambano huo dhidi ya timu ya zesco ya zambia kesho sa 10 jioni  uwanja wa amani   na kwamba wanaupa  mchezo huo umuhimu mkubwa kutokana  na kiwango cha timu wanayocheza nayo

Kwa upande wake nae kocha wa timu ya zesco tenant chembo amesema wanaiheshimu timu ya jku kutokana na aina ya wachezaji iliyokuwa nayo na  vipaji vyao  na kwamba  wao wamejipanga vyema kupata matokeo mazuri hapo kesho

Bakari ali cheupe ni afisa wa habari wa chama cha soka zanzibar zfa  na hapa anaelezea kuhusiana na kukamilika kwa maandalizi ya michezo hiyo ikiwemo kuwasili kwa waamuzi watakao chezesha  mitanange hiyo

Wakati huo  huo nayo timu ya zimamoto imeendelea na mazoezi ya mwishomwisho kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho afrika dhidi ya timu ya  walaita dicha ya ethiopia utakaopigwa jumapili saa 10 jioni

Zbc imetembelea mazoezi ya timu hiyo uwanja wa amani na kufanikiwa kuzungumza na nahodha wa timu hiyo hassan saidi hassan huku akisema hawatakubali kufanywa  njia ya mkato na wapinzani wao.

Nae kocha wa kikosi hicho amesema hadi sasa hakuna mchezaji aliyekuwa  majeruhi katika kikosi chao huku wachezaji wote wakiwa na morali ya kushinda mchezo wao