TRA IHAKIKISHE INAWEKA UTARATIBU WA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA MARA KWA MARA

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. Samia suluhu hassan amemwagiza kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato tanzania (tra) ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero zinazowakabili wafanyabiashara hao
Akizungumza na kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato tanzania (tra) charles kichere mh samia amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Makamu wa rais amesikitishwa na baadhi ya maafisa wa tra kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali inayosababisha malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara na kutaka likatafutiwa ufumbuzi.
Ameisisitiza tra kuwa ni muhimu iwapo itafanya mabadiliko yoyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi.
Makamu wa rais pia ameipongeza tra kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na kuitaka iongeze bidii katika ukusanyaji wa kodi ambazo serikali inatumia katika mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake, kamishna mkuu wa tra nchini charles kichere atayafanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wafanyabiashara na kuwachukulia hatua stahiki wanaokiuka maadili ya kazi