TRA IMEFANIKIWA KUKUSANYA SHILINGI TRIONI 14 NUKTA 4

Mamlaka ya mapato tanzania (tra) imefanikiwa kukusanya shilingi trioni 14 nukta 4 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam na mkurugenzi wa huduma ya elimu kwa mlipa kodi richard kayombo amesema makusanyo hayo yameongezeka kwa asilimi 7.76 ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka wa fedha 2015/16 ambapo yalikuwa shilingi trioni 13.3.
Aidha kayombo ametoa wito kwa wafanya biashara kutoa risiti za efd pindi wanapo uza bidhaa au kutoa huduma huku wananchi wakitakiwa kudai na kukagua risti zao mara baada ya kununua bidhaa zao.
Hata hivyo nd. Kayombo amewataka wananchi kuendea kulipia kodi ya majengo ili kuondokana na usumbufu utakao jitokeza