TRILIONI MOJA NA BILIONI 87 MWAKA WA FEDHA 2017/2018

 

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imekadiria kutumia kiasi cha shilingi trilioni moja na bilioni 87 nukta nne katika mwaka wa fedha 2017/2018 ikiwemo matumizi ya kawaida na maendeleo.

Waziri wa fedha dk khalid salum mohamed amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 675 nukta nane zinatarajiwa kukusanywa kwa mwaka huo kutoka vyanzo vya ndani ikiwemo zrb iliyopangiwa kukusanya shilingi bilioni 258 nukta tatu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu muelekeo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha amevitaja vipaumbele kwa mwaka huo wa fedha  ni kuimarisha ubora wa huduma za kijamii ikiwemo elimu, maji safi na huduma za afya, miundo mbinu ya bandari na uwanja wa ndege, ujenzi wa barabara na nishati.

Waziri khalid amevitaja vipaumbele vingine kuwa ni uimarishaji wa sekta ya utalii na viwanda vidogo ili kuimarisjha sekta ya ajira pamoja na mpango wa ununuzi wa meli ya abiria na mafuta.

Aidha amefahamishakuwa serikali inatarajia kupokea shilingi bilioni 380 nukta tano kutoka kwa washirika wa maendeleo za zuruku na mikopo.

Kuhusu kodi waziri khalid amesema serikali   katika kipindi hicho haitapokea misaada ya kibajeti wala kupandisha kodi ya aina yoyote badala yake itaimarisha zaidi ukusanyaji wa mapato.