TRUMP AENDELEA NA ZIARA YAKE BARANI ASIA AMBAPO YUPO NCHINI CHINA

 

Rais wa marekani donald trump anaeendelea na ziara yake barani asia ambapo yupo nchini china na anafanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo xi jinping, akijikta zaidi juu ya kitisho cha nyuklia cha korea kaskazini.

Trump amesema hatoruhusu miji ya marekani kutishiwa na makombora hatari ya korea kaskazini.

Katika hotuba yake kwa bunge la korea kusini trump amesema marekani haitafuti migogoro au makabiliano lakini pia kamwe haitokimbia hali hiyo na haiko tayari kuruhusu ishambuliwe au washirika wake kushambuliwa

Aidha trump ametoa wito wa kuwepo mshikamano kimataifa dhidi ya korea kaskazini iliyotengwa.