TRUMP ALIHUTUBIA BUNGE

 

Rais wa marekani donald trump ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa yuko wazi kuhusu mageuzi ya uhamiaji.Katika hotuba hiyo trump ameweka kando tofauti zake na wademocrats na vyombo vya habari na kutoa hotuba inayolenga kurejesha imani ya wamarekani wanaokerwa na uongozi wake.Kiongozi huyo anataka yafanyike mageuzi katika mfumo wa afya, utozaji mkubwa wa kodi, mpango wa umma na sekta ya kibinafsi .

trump amewataka warepublican na wademocrat kushirikiana kuhusu mageuzi ya sera ya uhamiaji na kuahidi mwamko mpya wa marekani.