TRUMP AMTIMUA MKURUGENZI WA FBI JAMES COMEY

 

Ikulu ya white house imetangaza kuwa rais wa marekani donald trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la upelelezi – fbi james comey kuhusiana na namna alivyoshughulikia suala la barua pepe za hillary clinton.

Comey alikuwa akisimamia uchunguzi kuhusiana na mawasiliano kati ya viongozi wa kampeni ya trump na maafisa wa urusi kabla ya uchaguzi wa rais mwaka wa 2016.

raisi donald trump amesema katika barua yake kuwa tayari anamtafuta mtu atakayechukua nafasi ya comey.