TRUMP ANATAKA VIKWAZO ZAIDI KWA KOREA KASKAZINI

 

Rais wa marekani  Donald Trump ametoa wito kwa korea kaskazini kuwekewa vikwazo vikali zaidi baada ya jaribio lake la kombora la masafa marefu hii leo pamoja na kitisho dhidi ya kiongozi mpya wa kiliberali wa korea kusini.

katika taarifa yake ikulu ya marekani imesema uchokozi huo wa sasa utumike kama wito kwa mataifa yote kuweka vikwazo madhubuti dhidi ya korea kaskazini.

Kombora hilo lilirushwa umbali wa kilometa 700 kabla halijatua katika bahari ya japan.

awali rais trump alitishia kuchukua hatua kali za kijeshi lakini baadae akalegeza msimamo wake kwa kusema yupo tayari kukutana na rais wa korea kaskazini kim jong un kwa mazungumzo