TRUMP ASEMA MATAIFA MAWILI SIO SULUHISHO PEKEE KATI YA ISRAEL NA PALESTINA

Rais wa Marekani Donald Trump amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jana mjini Washington. Viongozi hao walisema wana uhakika uhusiano kati ya nchi zao utapiga hatua mpya, huku kukiwa na minong’ono kuwa Trump atafanya mabadiliko makubwa katika sera ya Marekani kuhusu eneo la Mashariki ya Kati. Katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Trump alisema yeye atakaribisha suluhisho lolote katika mzozo kati ya Israel na Palestina, liwe la mataifa mawili au la taifa moja, mradi likubaliwe na pande zinazohusika. Netanyahu kwa upande wake ameelezea matumaini mema kutoka utawala mpya wa Marekani kuelekea Israel, akisema amefurahia wito wa utawala huo kuhakikisha Israel inatendewa haki katika jukwaa la kimataifa, na kwamba Marekani itatumia nguvu zake kupinga ususiaji dhidi ya Israel