TRUMP ATOA MASHARTI MAPYA YA USAFIRI KWA NCHI 6 ZA KIISLAMU

Utawala wa Rais Trump umeweka masharti mapya ya maombi ya visa kutoka kwa mataifa sita ya kiislamu pamoja na wakimbizi wote, ambayo yanawataka kuwa na mtu wanaohusiana ama ushirikiano wa Kibiashara na Marekani.

hatua hiyo inayoyahusisha mataifa ya Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen.

masharti hayo mapya yalioanza kufanya kazi siku ya alhamisi yanaelezea mahusiano ya kifamialia.

masharti hayo yamekuja baada ya mahakama kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la Rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa waislamu.