TRUMP AZUNGUMZA NA ABE NA XI KUHUSU KOREA KASKAZINI

Rais wa marekani donald trump amezungumza na rais wa china xi jinping na waziri mkuu wa japan shinzo abe kuhusu korea kaskazini
Mazungumzo hayo ya simu yanafanyika huku kukiwa na hali ya wasi wasi kuwa korea ya kaskazini inaweza kufanya jaribio la makombora ya kinyuklia wiki hii.
xi amemtaka trump kuwa na uvumilivu huku akieleza kuwa china inapinga ukiukaji wa maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa na ina matumaini pande zinazohusika zitajiepusha kuendeleza hali ya wasi wasi katika rasi ya korea.
korea kaskazini imesema iko tayari kuzamisha meli ya kivita ya marekani baada ya meli kadhaa za marekani kuruhusiwa kuingia katika eneo la maji la rasi ya korea.