TTCL IMEZINDUA HUDUMA MPYA ZA MAWASILIANO YA INTANENTI

 

 

kampuni ya simu tanzania ttcl imezindua huduma mpya za mawasiliano ya intanenti zenye muda wa kutosha kupiga simu zilizo na bei nafuu kwa wateja wake.

akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini dar es salaam kaimu afisa mkuu masoko na mauzo ttcl, laibu leonard amesema uzinduzi huo utakuwa chachu kwa wanaanchi kurudia kutumia mtandao wao wa ttcl kutokana na unafuu wa mahitaji ya matumizi yake.

ameelezea kuhusu mkakati wa mageuzi wa kibiashara utakaohusu mabadiliko ya kuboresha mwelekeo wa ttcl kibiashara na kuirejesha kampuni hiyo kuwa kiongozi wa huduma za mawasiliano ndani na nje ya mipaka ya tanzania.

vifurushi vilivyozinduliwa ni kifurushi cha bandika bandua, t connect plus, kifurushi cha waandishi wa habari, kifurushi cha nyumbani pack, bussiness pack, na kifurushi cha office connect pack.