TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UKAHABA

 

 

Serikali ya mkoa wa mjini magharibi imefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watu 20 kwa tuhuma za  kujihusisha na biashara ya ukahaba katika maeneo ya mkoa huo.

Watuhumiwa hao wamekamatwa majira ya saa 4 hadi 6 za usiku katika nyumba ya kulaza wageni new happy iliyopo michenzani na burudani bar iliyopo kilimani kwa raju, ambapo watuhumiwa hao walikutwa wakiwa katika harakati za kufanya biashara hiyo.

Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mhe ayuob mohammed mahmoud aliongoza operesheni hiyo ambapo amesema wamechukuwa hatua hiyo kufuatia taarifa za kufanyika vitendo vya ukahaba katika maeneo hayo licha ya serikali kupiga marufuku  vitendo hivyo.

Katika hatua nyengine mkuu wa mkoa ameifungia nyumba ya kulaza wageni ya new happy kutokana na kutumika kama danguro na kuliagiza baraza la manispaa ya mjini kuifutia leseni baada ya kukiuka taratibu za uendeshaji wa biashara hiyo.

Nae mkuu wa wilaya ya mjini marina joel tomas ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa ili kurejesha nidhamu katika mkoa huo